KOCHA JOACHIM LOW APONGEZA KIKOSI CHAKE KUICHAKAZA SAN MARIO

MABAO matatu ya mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Serge Gnabry yalisaidia Ujerumani kuichakaza San Mario maba 8-0 kwenye mechi ya makundi ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia.

Ujerumani imeanza vizuri kampeni ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia kwa kushinda mechi nne mfululizo.

Kocha wa Ujerumani Joachim Low alikuwa bila nyota wake sita wakiwamo Jerome Boateng, Manuel Neuer na Toni Kross.

Alitoa nafasi kwa winga wa Werder Bremen Gnabry kuchezea kikosi hicho kwa mara ya kwanza.


“Nimefurahi kuona wachezaji wangu wamecheza kwa uchu wa kusaka mabao,” alisema Low wakati akizungumza na waandishi wa habari.

No comments