KOCHA UFARANSA ATAKA KIKOSI CHAKE KIJIFUNZE MBINU ZA KUZIKABILI TIMU ZINAZOCHEZA KWA "KUPAKI BASI"

KOCHA wa Ufaransa, Didier Deschamps amesema kikosi chake kinapaswa kiujifunza kucheza dhidi ya timu zinazocheza kwa ‘Kupaki basi’.

Ufaransa juzi iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Sweden kwenye mechi ya kuewania kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia.

Ilipata wakati mgumu kwenye mechi hiyo na Sweden na mchezo ulikuwa mgumu zaidi wakati Ufaransa ilipopata bao la kuongoza kupitia Emil Forsberg.


Ufaransa ilipata mabao yake kupitia kwa Paul Pogba na Dimitri Payet.

No comments