KOCHA WA BARCELONA AWAJIA JUU AKINA MESSI KWA KUONYESHA KIWANGO KIBOVU

KOCHA wa Barcolona Luis Enrique aliwapandishia nyota wake baada ya kufungana mabao 1-1 na Real Sociedad kwenye mechi ya La Liga Jumapili iliyopita.

Enrique aliitisha kikao na nyota walioongozwa na Lionel Messi na kueleza wazi jinsi asivyofurahishwa na kiwango cha timu hiyo katika siku za karibuni.

Aliitishakikapo dakika ya 15 kabla ya mazoezi ya timu hiyo kutokana na kuwa pointi sita nyuma ya Real Madrid kwenye msimamo wa Ligi.


Barcelona inakabiliana na wapinzani wao wa jadi Real Madrid Jumamosi kwenye mechi inayosubiriwa kwa hamu duniani kote.

No comments