KOCHA WA PSV AKIMIMINIA SIFA KIKOSI CHA DIEGO SIMEONE

KOCHA wa timu ya PSV Phillip Cocu amekisifia kiwango kilichoonyeshwa na wapinzani wa Atletico Madrid akisema kuwa ni mfano wa jinsi timu inavyotakiwa kucheza na ndio maana wakafungwa katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa uliopigwa usiku wa kuamkia juzi kwenye uwanja wa Vicente Calderon.

Walikuwa ni wachezaji Antoine Griezmann na Kevin Gameiro ndio walioipatia timu yao mabao vijana hao wa Diego Simeone na hivyo kuwafuta machozi ya kipigo walichokipata mwishoni mwa wiki kutoka kwa mahasimu wao Real Madrid na huku wakishika nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa michuano ya Kundi D.

Kutokana na kiwango hicho, Cocu anasema kuwa licha ya kuwa walicheza vizuri lakini walikuwa na uwezo mdogo wa kuzima mashambulizi ya wapinzani wao.

“Tulitarajia Nicolas Gaitan atacheza pembeni lakini hakucheza,” kocha huyo aliwaambia waandishi wa habari. “Walijipanga kwa njia nyingine.”


“Walicheza mfumo mwingine ambao uliwafanya kutufunga mara mbili kabla hatujajipanga,” aliongeza kocha huyo.

No comments