LULU AFUNGUKA KUHUSU KUGOMA KUFANYA "VIDEO QUEEN"

STAA wa Bongomuvi, Elizabeth Michael “Lulu” ametoa sababu ya kukataa ofa ya kupamba video za wasanii (Video Vixen) na kuweka wazi kwamba yeye ni mwigizaji sio mwanamuziki.

Kimwana huyo ambaye siku za nyuma aliwahi kushiriki katika video ya wimbo wa Linex, alisema kuna wasanii wengi tu wa muziki wa kizazi Kipya nchini na nje ya nchi ambao wamekuwa wakitamani kumshirikisha katika video za nyimbo zao lakini hayuko tayari.

“Kuna wasanii ambao walishaniomba kwa kunipigia simu na wengine huwa ninasoma kwenye vyombo vya habari wakisema niwe video Queen kwenye nyimbo zao, lakini siko tayari kwasababu mimi so mwanamuziki,” alisema Lulu.


Alisema kuwa anataka kutumia muda mwingi kuboresha fani yake ya uigizaji na sio kuelekeza nguvu kwenye kazi za swengine ikiwemo hiyo ya kushiriki katika video za wasanii wa muziki wa Kizazi Kipya.

No comments