MACHO YOTE MIAKA 30 YA ALLY CHOCKY KWENYE MUZIKI WA DANSI JUMAMOSI HII MANGO GARDEN


Joto la tamasha la kuadhimisha miaka 30 kwenye  muziki wa dansi kwa mwanamuziki Ally Chocky limeanza kupanda baada ya nguli huyo kuingia kambini na magwiji wenzake.

Magwiji watakaoungana na Ally Chocky katika onyesho hilo la aina yake ni Komandoo Hamza Kalala,Tshmanga Kalala Assosa na Zahir Ally Zoro.

Akizingumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam wiki hii, Chocky alisema ameingia kambini kuanza mazoezi na magwiji hao katika nyimbo zote alizofanya nao mwanzo wa safari yake ya maisha ya muziki.

Onyesho la miaka 30 ya Chocky katika muziki wa dansi litafanyika Mango Garden Jumamosi hii na kusindikizwa na Twanga Pepeta, Msondo Ngoma na Msagasumu.

No comments