MADAKTARI WAIHAKIKISHIA LIVERPOOL MAJERUHI COUNTINHO ANA WIKI TANO TU NJE

LIVERPOOL imeweka matumaini yake vizuri baada ya kufahamu kiungo wake Philippe Countinho atakuwa nje kwa wiki tano hadi sita.

Kufuatia tathmini ya madaktari imeonekana majeraha yake ya enka sio makubwa kama ilivyothaniwa awali.

Vipimo vimeonyesha kuwa halazimiki kufanyiwa upasuaji na anatazimiwa kurudi uwanjani katikati ya mwezi Januari.

Countinho aliumia baada ya kugongana na Didier N’dong wa Sunderland wikiendi iliyopita.

Liverpool hata hivyo itakuwa imepata pigo kutokana na kumkosa nyota huyo wakati wa ratiba ngumu ya sikukuu.

“Phil amefaniwa vipimo na tunatarajia kuwa hatakuwa muda mrefu nje ya uwanja,” alisema kocha wa Liverpool Jurgen Klopp.


Countinho ni mchezaji muhimu kwa Liverpool katika harakati zake za kutwaa ubingwa msimu huu.

No comments