MAJANGA YAENDELEA KUMWANDAMA JOSE MOURINHO... atakiwa kujieleza baada ya kupewa kadi nyekundu

NI kama mwendelezo wa majanga. Bosi wa Manchester United ameingia tena matatani kwa mara ya pili ndani ya wiki moja, safari hii akitakiwa kujieleza baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu kwenye mechi ya bila kufungana ya Ligi Kuu ngland dhidi ya Burney Jumamosi iliyopita.

Alhamisi iliyopita chama cha soka England (FA), kilimtia hatiani kocha huyo Mreno na kumtaka kujieleza kutokana na kauli aliyoitoa akimlenga mwamuzi Anthony Taylor.

Anatuhumiwa kutumia aidha lugha ya matusi au maneno makali dhidi ya mwamuzi wa mechi hiyo wakati wa mapumziko. Amepewa hadi Ijumaa kujieleza.

FA imechukua hatua hiyo bada ya kupitia ripoti ya mwamuzi Clattenburg iliyopendekeza hatua kuchukuliwa dhidi ya kocha huyo ikiwemo kupigwa faini au kuzuiwa kukaa kwenye benchi.


Mourinho alionekana kukasirishwa vikali baada ya United kunyima penati kutokana na Jon Flanagan kumchezea vibaya Matteo Darmian ndani ya boksi la hatari.

No comments