MAJERUHI ALEXIS SANCHEZ AMTIA MCHECHETO KOCHA ARSENE WENGER

HOFU imetanda katika klabu ya Arsenal kufuatia habari kwamba mshambuliaji wake Alexis Sanchez amepatwa na majeraha ya kiazi cha mguu akiwa katika ya timu ya taifa lake la Chile ambayo inajiandaa na michezo ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia.

Taarifa zilizothibitishwa na nchini Chile zimeeleza kuwa mshambuliaji huyo atafanyiwa vipimo hii leo ili kujua kama ataweza kuuwahi mchezo dhidi ya Colombia na kisha Uruguay.

Kitengo cha utabibu ambacho kipo nchini ya shirikisho la soka nchini Chile kimepewa jukumu la kuhakikisha majibu ya vipimo vya Sanchez yanapatikana haraka iwezekanavyo.

Hata hivyo Sanchez ataendelea kubaki mjini Santiago kwa ajili ya matibabu ya awali na kama mambo yataendelea kuwa tofauti na kufikia hatua ya kushindwa kujumuika na wenzake kwenye michezo hiyo miwili atalazimika kurejeshwa jijini London katika klabu yake ya Arsenal.

Taarifa za kuumia kwa Sanchez zinaweza zikawa pigo kwa meneja wa Arsenal, Arsene Wenger ambaye kwa sasa anaupigia hesabu mchezo ujao wa Ligi Kuu ya soka nchini England ambapo The Gunners watasafiri kuelekea mjini Manchester kwa ajili ya kupambana na Manchester United Novemba 19.

Kocha wa klabu hiyo Arsene Wenger amesema kwamba anataka kupata taarifa mapema kama kweli mchezaji huyo ameumia kwa kiwango kikubwa lakini kama majeraha yake ni ya kawaida ajue pia cha kufanya.


“Nataka kuona kwamba nitafanyaje katika mchezo ujao dhidi ya Man United maana najua kabisa kwamba Arsenal ni timu kubwa lakini ninajua kwamba nakabiliwa na mchezo mkubwa dhidi ya Man United,” amesema.

No comments