MAJERUHI DIEGO COSTA AZUA PRESHA KUBWA CHELSEA

DIEGO Costa ameumia na sasa atakuwa nje ya dimba kwa siku zisizofahamika hatua ambayo imezua presha ndani ya kikosi cha Chelsea.

Kuumia kwa straika huyo kulilipotiwa na uongozi wa timu ya taifa ya Hispania ambayo inajiandaa na mechi ya kimataifa dhidi ya Macedonia na England.

Hatua hiyo inamfanya Diego kuondolewa katika orodha ya wachezaji wa timu ya taifa ya Hispania lakini hofu kubwa ipo kwa timu yake ya Chelsea inayohofu kukosa huduma yake.

Diego mwenye umri wa miaka 28 kwa sasa anaongoza msimamo wa wafungaji wa Ligi ya premier na kocha wa Chelsea Antonio Conte amesikika akisema kuumia kwa straika huyo ni pigo kubwa.

“Nimepokea taarifa za kuumia kwake kwa masikitiko makubwa. Tutamkosa katika michezo kadhaa ijayo hatua ambayo ni mbaya kwetu.”


“Ukimkosa mchezaji wa kiwango chake ni dhahiri kuwa ni pigo na hili linamaanisha lazima tujipange tukiwa hatunaye ndani ya kikosi” amekiri Conte.

No comments