MAJERUHI FELLAINI JANGA LINGINE MANCHESTER UNITED... kukosa mechi ya wikiendi ijayo ndidi ya Arsenal

BALAA linaendelea kumwandama kocha wa Manchester United Jose Mourinho kutokana na kiungo wake Marouane Fellaini kuumia mguu na kumfanya kukosa mechi ya wikiendi ijayo ndidi ya Arsenal.

Fellaini aliumia sehemu ya nyuma ya moja ya miguu yake wakati Manchester United ilipoibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Swansea City lakini ilijiunga na kikosi cha Ubelgiji.

Hata hivyo kiungo huyo alikosa mechi ya kirafiki dhidi ya Uholanzi Jumatano iliyopita na hatacheza leo dhidi ya Estonia.

Ubelgiji huwa na kawaida ya kuita wachezaji wake hata kama  wameumia na mara ya kwanza ilidhaniwa Fellaoin hakuwa na majeraha ya kumkosesha mechi.


Fellaini ataongezeka kwenye orodha ya majeruhi wa Manchester United na kuungana na Antonio Valencia na Eric Bailly.

No comments