MAJERUHI FRANCESCO TOTTI AKARIBIA KUREJEA UWANJANI

STRAIKA mkongwe Francesco Totti anakaribia kurejea uwanjani baada ya kuanza mazoezi na kikosi cha timu yake ya Roma.

Totti alikuwa nje ya uwanja akikabiriwa na matatizo ya misuli ya nyama za paja katika mguu wake wa kushoto, hali iliyomfanya azikose mechi dhidi ya timu za Empoli, Austria, Vienna na Bologna.

Hata hivyo, sta huyo mwenye umri wa miaka 40 alirejea mazoezini hivi karibuni na kutumia mtandao wake wa facebook kuelezea furaha yake.


Hadi sasa Totti ameshafunga mabao mawili katika mechi sita alizokwishacheza katika michuano ya serie A.

No comments