MALKIA LEYLA RASHID APATA MSIBA MKUBWA ...AFIWA NA KAKA YAKE WA KWANZA


KAZI ya Mungu ina siri kubwa. Malkia Lelya Rashid Jumamosi alikuwa Mtwara kikazi, Jumapili akawa Lindi, Jumatatu akarejea Dar es Salaam lakini Jumanne akalazimika kurudi nyumbani kwao Mtwara baada ya kaka yake wa kwanza kuzaliwa kufariki dunia.

Mazishi ya kaka wa Leyla aitwae Mohamed Rashid (pichani kulia) yanafanyika  leo mchana huko huko Mtwara.

Shemeji wa marehemu Alhaj Mzee Yussuf ambaye naye yupo Mtwara kwenye msiba, ameiambia Saluti5 kuwa Mohamed aliugua malaria kwa siku chache na hali yake haikuwa na mashaka yoyote, lakini kazi ya Mungu haina makosa.

"INNALILAHI WA INNA ILAYHI RAJIOON"

No comments