MANCHESTER UNITED YAJIVUNIA MASHABIKI WA MITANDAONI

INAWEZEKANA bado sifa ya kujivunia nje ya dimba ambapo sasa klabu ya Manchester United wanajifariji kwa hatua ya kuwa na wafuasi wengi kupitia mitandao ya kijamii ikwemo ule wa Titter.

Haya yamebanishwa na mkurugenzi mkuu wa United, Richard Arnold.

Mkurugenzi huyo amenukuliwa akisema kuwa na wafuasi wengi kunatoa picha kuwa klabu hiyo inajulikana na wengi duniani kote na inawezekana ikafananisha na ufuasi wa kidini.

Alisema Arnold kuwa kwa sasa klabu ina mabilioni ya wafuasi wanaounganishwa na mitandao mbalimbali kiasi ambacho kinatia faraja ya kipekee.

“Kama ingekuwa ni dini nadhani klabu ina waumini wengi kote duniani, ni jambo linalotia faraja kwani ni hatua kubwa inayoiweka timu yetu juu ulimwenguni” alisema Arnold.

Alisema kwa mujibu wa takwimu inaonyesha kuwa United imefikisha wafuasi mil 9.22 wa mtandao wa Twitter ambapo katika mtandao wa Facebook kuna wafuatiliaji wanaofika 72.5.

Hii ni takwimu ya mwisho wa mwezi Novemba ya mwaka huu pekee.

Alisema hatua hiyo inamaanisha kuwa klabu ina wafuasi wanaomkaribia wale wa Justin bieber na Taylor Swift au Cristiano Ronaldo ambao ndiyo wanatajwa kuwa wafuasi na wengi katika mtandao wa Twitter kote duniani.


Ronaldo ndiye anayetajwea kuwa nambari moja kati ya wanandinga wenye wafuasi wengi duniani.

No comments