MANCHESTER UNITED YAKIRI KUCHEMSHA KUMFUKUZIA LIONEL MESSI

KLABU ya Manchester United imekiri kuwa imeshindwa katika mbio za kumwania straika Lionel Messi na huku ikiipa nafasi Man City kupata huduma ya nyota huyo endapo ataamua kuondoka Barcelona.

Kwa sasa nyota huyo mwenye umri wa miaka 29 yuko katika mvutano na labu yake kuhusu makubaliano ya kumpa mkataba mpya kutokana na kwamba anataka alipwe pauni 825,000 kwa wiki.


Hata hivyo, Man United wangekuwa na uwezo wa kumudu gharama hizo, lakini vigogo wake wanaamini ujio wa Pep uardiola ndicho kinachowafanya Man City kuwa na nafasi nzuri ya kumnasa nyota huyo.

No comments