MANCHESTER UNITED iko mawindoni kusaka saini ya kiungo wa Barcelona Ivan Rakitic ambaye bado ana mkataba wa kukipiga na klabu hiyo ya Camp Nou hadi mwaka 2019.
Nyota huyo wa kimataifa wa Croatia alijiunga na Barcelona mwaka 2014 akitokea Sevilla na kuwasaidia mabingwa hao wa Hispania kutwaa mataji matatu kwa mpigo (treble) - La Liga, Copa del Rey na Champions League ambapo alifunga bao la kuongoza kwenye fainali ya ushindi wa 3-1 dhidi ya Barcelona.
Barcelona inatarajiwa kuanzisha mazungumzo ya kurefusha mkataba wa Rakitic mwenye umri wa miaka 28 huku United ikijipanga kumdaka juu kwa juu iwapo nyota huyo atakataa kuongeza mkataba Camp Nou.
Kocha wa United Jose Mourinho anaamini Rakitic atakuwa pacha mzuri wa Paul Pobga kwenye safu ya kiungo.

NENDA PLAY STORE KUPITIA SMART PHONE YAKO KISHA DOWNLOAD APP YETU YA "SALUTI5">>>> BONYEZA HAPA
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac