MASHABIKI WA ENGLAND, SCOTLAND WAZICHAPA BAADA YA MCHEZO WAO

MASHABIKI wa England na Scotland juzi walipigana baada ya kumalizika kwa pambano la soka la kufuzu Kombe la Dunia.

England iliichakaza Scotland mabao 3-0 yaliyofungwa na Daniel Sturridge, Adam Lallana na Gary Cahill.

Scotland ilipoteza nafasi nyingi za wazi katika mchezo huo wa kuwania kufuzu kwa fainali.

Mchezo huo ulianza kwa utulivu kwa mashabiki wa timu hizo ndugu kutoa heshima kwa askari Uingereza waliokufa kwenye vita ya kwanza ya Dunia iliyotokea 1914-1918.


Hata hivyo wakati mchezo huo unakaribia kumalizika ndio ukazuka mzozo baina ya mashabiki wa timu hizo mbili na kuanza kupigana.

No comments