MASHAUZI CLASSIC KUIZINDUA RASMI KAOLE SNAKE PARK - BAGAMOYO LEO USIKU


KUNDI zima la Mashauzi Classic chini yake Isha Mashauzi “Queen of the Best Melodies”, leo usiku litaangusha burudani ya kukata na shoka mjini Bagamoyo eneo la Kaole.

Onyesho hilo la Mashauzi Classic litafanyika katika ukumbi wa Kaole Snake Park na huo ndio utakuwa uzinduzi rasmi wa ‘kiota’ hicho cha maraha.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotua Saluti5, mambo yataanza kunoga tangu mchana kwa burudani kadha wa kadha, vinywaji na nyama choma sambamba na michezo ya watoto, halafu usiku ndipo unapowadia ule wasaaa wa kula goma la Mashauzi Classic.

Kwa wale watakaofika tangu mchana watapata fursa ya kushuhudia nyoka wa kila aina wanaofungwa hapo Kaole Snake Park.


Isha Mashauzi ameiambia Saluti5 kuwa panapo na Mashauzi Classic basi huwa haliharibiki jambo …ni burudani bila kikomo.
Hii ndio Kaole Snake Park
 Isha Mashauzi anategemewa kusepa na kijiji huko Kaole leo usiku


No comments