MASHAUZI CLASSIC KUSHEREHEKEA MIAKA MITANO YA BENDI DISEMBA 1 MANGO GARDEN …Melody kusindikiza


KUNDI la Mashauzi Classic limetimiza miaka mitano tangu lizaliwe rasmi na litafanya onyesho maalum Disemba Mosi kusherehekea miaka hiyo mitano ya burudani bila kikomo.

Mkurugenzi wa bendi hiyo Isha Mashauzi “Queen of the Best Melodies”, ameiambia Saluti5 kuwa onyesho hilo litafanyika Mango Garden Kinondoni, Alhamisi ya kwanza ya mwezi Disemba.

Isha amesema kundi kongwe la East African Melody litasindikiza show hiyo ya aina yake.

Mashauzi Classic linatimiza miaka hiyo mitano bila kuterereka, bila kusimamisha maonyesho yao hata mara moja licha kuondokewa na wasanii wao kadhaa katika nyakati tofauti.

“Hii ni miaka mitano ya bila kikomo, hatujawahi kurudi nyuma, hatujawahi kusimamisha bendi, sio miaka mitano ya kuunga unga, hii ni kwasababu tumekuwa na mhimili mkubwa wa mashabiki waliojitoa kwa dhati kwetu”, alisema Isha.

No comments