MATONYA ASEMA MAMBO YA "KAMGAMBILE" HAYAPI NAFASI KWENYE MUZIKI WAKE

MATONYA amesema kuwa mambo ya “ndumba” hayana nafasi kwenye muziki wake kwa madai kwamba kuyatumia ni sawa na kujiharibia mbele ya mashabiki na kujikuta amepotea.  

“Katika maisha yangu huwa siamini ndumba na siwezi kuzipa nafasi kwa sababu kuziendekeza ni sawa na kujiharibia, ingawa wapo baadhi ya wasanii ambao wanadhani zinaweza kuwasaidia,” alisema Matonya.

Alisema kuwa jina lake limekuwa juu kwasababu ya ubora wa kazi zake na litaendelea kuwa juu bila kwenda kwa waganga na kuwashauri wanaoamini ni uchawi, kuachana na tabia hiyo.


“Braza, kwenye muziki kuna mambo mengi… wapo baadhi ya wasanii wanaoamini kwamba bila uchawi kazi zao haziendi na pia wapo wanaotumia uchawi kuwaharibia wenzao, lakini kwa ujumla ni kwamba huo wote ni upuuzi,” alisema mwimbaji huyo anayetambana wimbo “Sugua Benchi”

No comments