MESUT OZIL ASEMA ASEMA ALSENAL WAMEFUTA AIBU YA KIPIGO

MESUT Ozil alifunga bao la dakika za mwisho na kuwawezesha Arsenal kutoka nyuma 2-0 na kuwalaza Ludogorets Razgrad ya Bulgaria na kuwafikisha hatua ya mtoano wa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Ozil alionekana kutulia alipokimbia langoni akampiga chenga kipa na mabeki wawili na kisha akatumbukiza mpira kimiani kisha akasema wangelala ingekuwa aibu.

Awali matumani ya Arsenal kurudia ushindi wao mkubwa wa 6-0 mechi ya kwanza yalizimwa n Jonathan Cafu alipowaweka Ludogorets mbele baada ya free-kick ya Wanderson.

Cafu alisaidia ufungaji wa bao la pili alipomzidi ujanja Kieran Gibbs na kumpa mpira Claudiu Keseru aliyefunga na kuwashangaza Arsenal kwa bao moja.

Olivier Giroud naye alifunga kwa kichwa kutoka kwa mpira uliotoka kwa Aaron Ramsey na kusawazisha.

Kipa wa Arsenal, David Ospina alifanya kazi za ziada kuokoa mipira mara mbili kutoka kwa Wenderson kabla ya Ozil kufunga.

Baada ya mechi hiyo, Ozil amesema kwamba alijua kwamba watasawazisha ingawa muda ulivyokuwa unaenda waliona kama wataambulia kichapo.

“Muda wote tulikuwa tunajua tunatasawazisha lakini baadaye ikaonekana kama wapinzani wetu wamepania kutudhalilisha tukawa tunacheza kwa tahadhari kubwa. Tumefuta aibu ya kipigo” amesema.


Arsenal sasa wamefika hatua ya 16 bora na wameendeleza msululu wao wa kutoshindwa hadi mechi 15.

No comments