MICHAEL CARRICK ASEMA HUU NI MSIMU WAKE WA MWISHO MANCHESTER UNITED


KIUNGO mkongwe Michael Carrick amekiri kuwa huu unaweza ukawa msimu wake wa mwisho kuichezea Manchester United. 

Carrick ameanza katika mchezo mmoja tu wa Premier League msimu huu wakati kocha Jose Mourinho akipendelea zaidi kuwatumia Ander Herrera, Marouane Fellaini na Paul Pogba katika safu ya kiungo.


SAFARI YA SOKA LA MICHAEL CARRICK 

Umri: miaka 35
Timu:  West Ham  (1999-2004) - mechi 158, magoli 6

Tottenham (2004-2006)  - mechi 75, magoli 2 

Manchester United - (2006 - hadi sasa) - mechi 427, magoli 24 

Timu ya taifa England:  Mechi 34 

Mataji: Premier League 5, FA Cup 1, League Cup  2, Champions League 1,  FIFA Club World Cup 1
Hiyo inamaanisha kuwa Carrick, ambaye mwezi Julai atafikisha umri wa miaka 35, amekuwa akitumiwa kwenye mashindano mengine - EFL ambayo alianzishwa mara mbili na Europa League aliyoanzishwa mara moja - ingawa aliambualia kuanzishwa katika mchezo wa Premier League dhidi ya Swansea siku kumi zilizopita.

Soka alilolionyesha kwenye mchezo huo, linampa nafasi kubwa ya kuanza kwenye mchezo dhidi ya Arsenal Jumamosi hii, lakini Carrick anasema katika hatua hii ya soka lake, anaweza kukubali kwenda kutafuta changamoto mpya sehemu nyingine.

Michael Carrick has admitted this could be his last season as a Manchester United player

Michael Carrick amesema huu unaweza kuwa msimu wake wa mwisho Manchester United
The 35-year-old has won the FA Cup, the Champions League and five league titles with United

Michael Carrick akishangilia taji la FA na wachezaji wenzake

No comments