MIROSLAV KLOSE ASTAAFU SOKA... afungua milango ya ukocha timu ya taifa

MKONGWE wa Ujerumani, Miroslav Klose amesema sasa soka basi badala yake anafungua milango ya kuwa kocha wa timu ya taifa.

Klose aliyetangaza kustasafu soka badala ya kuiongoza Ujerumani kutwaa Kombe la Dunia mwaka 2014 hakuwa na timu ya kucheza tangu mara ya mwisho alipoachana na klabu ya Lazio.

Klose (38), pia aliwahi kukipiga na timu za FC Homberg, Kaiserslautern, Werder Bremen na Bayern Munch.

Bado anaendelea kuwa mfungaji bora wa wakati wote wa timu ya taifa ya Ujerumani akikwamisha kwenye kamba mabao 71 katika mechi 137.


Klose mwanasoka mwenye mafanikio makubwa Ujerumani anaachana na soka akiwa na rekodi ya ufungaji bora wa wakati wote fainali za Kombe la Dunia akifunga mabao 16 katika fainali nne.

No comments