SHOLO MWAMBA ADAI MASHABIKI WANAWAGOMBANISHA NA MAN FONGO

MKALI wa muziki wa Singeli Seif Mwinyijuma "Sholo Mwamba" amewataka mashabiki wake kuacha kusikiliza taarifa zinazoenezwa na wale wasiomtakia mema kwamba ana ungomvi na wasanii wenzake wa muziki huo.

“Sina ugomvi na mamnii yeyote na wala siuendekezi kwa sababu madhara yake ni makubwa na kama wapo wanaotumia njia hiyo kama kiki basi mashabiki wangu msikubaliane nao,” alisema Sholo.

Alisema kuwa tangu alipotoa ushauri kwa wasanii mwenzake Man Fongo kuwa akaze buti kwa kutoa nyimbo kali zaidi badala kutegemea “Hainaga Ushemeji" kumekuwepo na maneno kwamba wawili hao wana ugomvi.

“Mimi ni mtoto wa uswahilini na tabia yetu uswahilini sio kuwekeana visasi ama kuendekeza ugomvi ila nina amini kuna watu wanataka kutugombanisha ndio maana ninawaambia mashabiki wangu wasikubaliane na hilo,” alisema.   

No comments