MKONGWE JB KUTOSTAAFU TENA MWAKA HUU... asema atastaafu mwaka ujao akishatoa filamu yake ya mwisho

MWIGIZAJI wa Bongomuvi Jacob Stephen "JB" amesema kuwa alikuwa akitamani mwaka huu uwe wa mwisho kuigiza lakiniu mambo yamekwenda kinyume na alivyopanga.

Alisema kuwa sasa umebakia mwezi mmoja ambao siyo rahisi kuandaa filamu ikakamilika hivyo analazimika kustaafu mwaka ujao akishatoa filamu yake ya mwisho ili abaki kuwa mwongozaji tu.

“Ratiba yangu ilikuwa ni kwamba baada ya kutoa filamu ya "Kiu ya Kisasi" ningeandaa nyingine mwaka huu na kisha nistaafu lakini naona muda unakwenda mbio halafu sasa mwaka unaisha,” alisema JB.

No comments