MONALISA AKATAA SHAVU KWENYE MUVI ZA CHIPUKIZI ZISIZO NA UBORA

MKONGWE wa Bongomuvi, Monalisa ameweka wazi kuwa hayuko tayari kushirikishwa kwenye filamu za wasanii chipukizi ambazo zinaweza kumshusha hadhi yake.

“Ni lazima nijiridhishe kwanza kama filamu husika inaweza kuendelea kulinda hadhi yangu lakini nikibaini kwamba inaweza kuniharibia sitakuwa tayari kushirikishwa,” alisema Monalisa.

Msanii huyo alisema kuwa anatambua umuhimu wa kuibua vipaji lakini pia anazingatia umuhimu wa kulinda hadhi ya jina lake kwenye sanaa hiyo isipotee kwasababu ya kushirikishwa katika filamu mbovu.


“Ruksa msanii chipukizi kunishirikisha katika filamu iwapo tutakubaliana malipo lakini cha msingi ni kuangalia kazi yenyewe kama inaweza kuendelea kulinda hadhi ya jina langu,” alisema.

No comments