MR BLUE SASA AAMUA KUJIITA "NYANI MZEE"

RAPA mahiri Mr Blue amesema kuanzia sasa anataka ajulikane kwa jina la utani la "Nyani Mzee" badala la lile la awali alilokuwa akilitumia la "Smba" kuchukuliwa na Diamond Platnumz.

“Ukweli ni kwamba kwa sasa jina la "Simba" nimeliacha ila kwa sasa natumia jina la "Nyani Mzee" nikimaanisha nimekwepa mishale mingi nasubiri na hilo wachukue nitafute jina lingine,” alisema msanii huyo.

Mr Blue alikuwa akizungumza katika kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio, ambaye Desemba mwaka jana alikuwa katik mzozo na Diamond kuhusu jina la “Simba” huku kila mmoja akidai ni lake.

Mbali na hilo, msanii huyo alisema kuwa licha ya kukubalika kwa mashabiki wengi na kuwa kwenye tasnia ya muziki kwa muda mrefu, hajawahi kupata tuzo hata moja ya kutambua mchango wake kwenye muziki.


No comments