MUZIKI MNENE WA EFM UKO MANGO GARDEN JUMAMOSI HII …TWANGA YAENDA KIGAMBONI


ILE kampeni ya Muziki Mnene ya kituo cha radio EFM itakuwepo Mango Garden Kinondoni Jumamosi hii, huku wenyeji Twanga Pepeta wakielekea Kigamboni.

Twanga Pepeta ambayo kwa kawaida hupatikana Mango Garden kila Jumamosi, itakuwa na onyesho maalum ndani ya Liquid Pub Kigamboni Novemba 26.

Mmoja wa wakurugenzi wa Twanga Pepeta, Omar Baraka ameiambia Saluti5 kuwa onyesho hilo litakuwa ni la kusherehekea miaka miwili ya Liquid Pub.

No comments