MWANAMUZIKI ADELE ADKINS AZIDI "KUTISHA" KWA MSHIKO BARANI ULAYA


MWANAMUZIKI maarufu zaidi nchini Uingereza, Adele Adkins amezidi kutisha kutokana na kutangazwa kuwa msanii tajiri zaidi wa kike barani Ulaya kwa sasa.

Kwa mujibu wa gazeti la Britains’ Heat, limetoa ripoti hiyo kuwa kwa sasa Adele ana utajiri wa kufikia dola mil 111 ukilinganisha na mwaka jana ambapo alikuwa na utajiri wa dola 47 na kushika nafasi ya 43 kwa matajiri wanawake duniani.

Mwimbaji huyo ameongoza orodha hiyo kutokana na kuingiza fedha nyingi kutoka kwenye mauzo ya albamu zake na dili za matangazo mbalimbali alizokuwa nazo.


Mbali ya Adele, wasanii wengine kwenye orodha hiyo ni Daniel Radeliffe dola mil 91.6, Harry Potter na Ed Sheeran dola mil 55.8, Zayn Malik dola mil 47.1, Harry Styles dola mil 45.8. Emma Watson dola mil 43.3, Harry Potter na Liam Payne dola mil 42.1 na Niall Horan dola mil 42.1.

No comments