MWANZO MBAYA WA RIYAD MAHREZ WAMPASUA KICHWA CLAUDIO RANIERI

KOCHA wa Leister City Claudio Ranieri ameeleza jinsi anavyoumia kichwa akitafuta njia ya kumsaidia straika wake Riyad Mahrez baada ya kuwa na mwanzo mbaya msimu huu na huku klabu yake ikiendelea kuwa katika wakati mgumu katika mbio za kutetea ubingwa.

Mchezaji bora huyo wa mwaka wa chama cha wanasoka wakulipwa (PFA), akiwa na Leicester City aliushangaza ulimwengu kwa kuwezesha timu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu uliopita lakini kwa sasa Mahrez anaangaika kurejea katika ubora wake na huku mabingwa hao watetezi wakiwa nafasi ya 14 kwenye misimamo ya michuano hiyo.

Jumamosi Mahrez alifunga mkwaju wa kwanza wa penalti lakini ukawa ni mchezo mwingine mbaya kwa Leister City baada ya kuambulia kipigo cha mabao 2-1 kikiwa ni cha sita.

Kutokana na hali hiyo Ranieri anapima upepo ili kuona aidha amuondoe kwenye orodha ya kikosi chake mchezaji huyo ambaye yupo kwenye orodha ya wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa Dunia Ballon D'Or, zikiwa ni jitihada za kumsaidia arejee kwenye ubora wake.

“Ni sawa tunahitaji kufanya kitu fulani, nafanyia kazi kitu fulani kwa sababu wapinzani wetu kwa sasa wanatufahamu vizuri na hatuwezi kuendelea na Riyald pekee na kumkabidhi majukumu yote."


"Unaweza kuangalia mechi na kila wakati Riyad anakuwa akipata mpira anakuwa akitaka kufanya kitu cha aina ya kipekee lakini wapinzani wanakuwa katibu naye,” aliongeza kocha huyo.

No comments