MWIGIZAJI HILDA DOKUBO WA NIGERIA ACHEKELEA MIMBA ALIYOIPATA AKIWA NA UMRI WA MIAKA 17

MWIGIZAJI mkongwe Hilda Dokubo amefunguka kwamba mimba aliyoipata akiwa mtoto wa miaka 17 imebadilisha maisha yake.

Dokubo aliueleza mtandao wa Najistic.com hatua ya kubadilika kwa maisha yake inatokana na mwanaume aliyempa ujauzito huo kukubali kuulea.

Alisema kwamba anashukuru licha ya kutokea kwenye familia yenye msimamo wa kidini lakini hawakumfukuza wala kumsema vibaya bali walimshauri na kumuandaa kisaikolojia.


“Hivyo hata mimi sikujisikia vibaya kwakuwa aliyenipa ujauzito alikubali kunioa pamoja na kuniendeleza kwa mambo mengine ikiwemo elimu,” alisema.

No comments