MZEE YUSSUF NA ISHA MASHAUZI USO KWA USO NDANI YA MWANZA


MTU na ‘mwanae’ - Mzee Yussuf na Isha Mashauzi wamekutana jijini Mwanza na kubadilishana mawazo kadha wa kadha sambamba na kupata mlo wa mchana pamoja.

Mzee Yussuf ambaye ni mwanamuziki mstaafu wa taarab, ndiye aliyemtungia Isha Mashauzi wimbo wake wa kwanza wa taarab “Hayanifiki” enzi hizo wakiwa ndani ya Jahazi Modern Taarab miaka 10 iliyopita.

Isha na Mzee Yussuf wamekuwa wakipeana heshima ya mtu na baba yake kutokana na namna walivyoleana katika kazi ya muziki wa taarab.

Isha yupo jijini Mwanza kwaajili ya onyesho la “Sauti ya Mwanamke” huku Mzee Yussuf akiwa jijini humo kwa ziara ya kidini.
 Mzee Yussuf haishiwi mzaha, hapa akimchekesha Isha kupita maelezo
  Mzee Yussuf akiendelea kumvunja mbavu Isha
   Mzee Yussuf katika mlo wa nguvu
Isha Mashauzi na Mzee Yussuf wakiwa jijini Mwanza Jumamosi jioni

No comments