NAJMA DATTAN, BARAKAH DA PRINCE WAWAPASHA WANAOWAFUATILIA WASITAFUTE KIKI KUPITIA PENZI LAO

MWAMBAJI wa Kizazi Kipya, Najma Dattan Naj ameibuka na kusema hana muda wa kujibizana na wale wanaomfuatilia uhusiano wake na Barakha Da Prince akidai wanahangaika tu.

Alisema kwamba watu wawili wanapokubaliana kuwa na mahusiano ya kimapenzi wanajua wenyewe ni kwa nini wamefikia hatua hiyo wala mtu mwingine hana nafasi ya kuhoji.

“Wanaonisema niwaambie kuwa wanahangaika tu kwa sababu sisi wenyewe tumependana na niseme kuwa kwa Barakah nimefika kwani ninalikubali penzi lake,” alisema Najma.

Kwa upande wake Barakah alisema kuna baadhi ya wasanii wamekuwa wakitafuta "kiki" kwa kutumia uhusiano wake na Najma lakini wataambulia patupu.

Alisema kuwa uhusiano wao ni wa kweli na ndiyo maana alimchukua Najma na kwenda kumtambulsha kwa wazazi wake jijini mwanza.


“Wenye wivu wajinyonge na wala wasitafute kiki kwa kutumia uhusiano wetu kwani wataendelea kusuburi sana wakati sisi tukifurahia mapenzi yetu,” alisema Barakah.

No comments