NDOA YA JADO FFU NA DAR MUSICA YAVUNJIKA …wenye bendi wadai wamemtimua, mwenyewe asema amejiengua


UONGOZI wa bendi ya muziki wa dansi ya Dar Musica, umemfukuza kazi aliyekuwa aliyekuwa Rais wa bendi hiyo Edward Anthony 'Jado Field Force' (pichani juu) kwa utovu nidhamu.

Akizungumza na Saluti5 mtendaji wa bendi hiyo Jumanne Mndia alisema kuwa uongozi wa bendi hiyo umeamua kufanya hivyo baada ya Jado kushindwa kumudu vyema majukumu yake na kufikia hatua ya kuanzisha makundi miongoni mwa wanamuziki na kuigawanya bendi yao.

Mndia amesema jana mchana walimpatia Jado barua rasmi ya kumuondoa ili aweze kuwa huru kutafuta sehemu ya nyingine ya kwenda kufanya.

Jado Field Force ni miongoni mwa wanamuziki kutoka katika bendi ya Mashujaa ambao walijiunga na Dar Musica chini ya mkurugenzi wake Ramadhan Mkoka na hatimaye kufanya uzinduzi wake rasmi Septemba 16 mwaka ndani ya Mango Garden jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, jana majira ya saa 4 usiku, Jado alitoa tamko kupitia ukurasa wake wa Facebook akidai amejiuengua Dar Musica baada ya kushindwana na mmiliki mwenzake kwenye utaratibu wa kuendesha bendi.

Jado akasema mwenzake alileta vyombo, yeye akakusanya wanamuziki lakini sasa mmiliki mwenzake huyo kamgeuka na anamwachia Mungu.
Hiki ndicho alichoweka Jado kwenye ukurasa wake wa Facebook

No comments