NISHA ASEMA KUHESHIMU MASHABIKI NDIO SIRI KUBWA YA MSANII KUFANIKIWA

SALMA Jabu “Nisha” amesema kuwa siri kubwa inayoweza kumfanya msanii kupata mafanikio makubwa ni kuheshimu mashabiki wanaomweka mjini vinginevyo haezi kufika kokote.

“Kwa msanii anayejua umuhimu wa hilo hawezi kudharau mashabiki wake hata siku moja kwa sababu ndio wanaomfanya azidi kujulikana lakini ajabu ni kwamba miongoni mwetu wapo ambao wanadharau mashabiki,” alisema Nisha.

Heshima hiyo inaambatana na kusikiliza maoni yao na kuyafanyia kazi kama kutakuwa na haja hiyo kutokana na ukweli kwamba ndio wanunuzi wakubwa wa filamu.


“Mimi ninalitambua hilo na ndio maana ninaendelea kupata umaarufu kwasababu ninawaheshimu watu hawa ambao kimsingi ndio walioniweka mjini, siwezi kuwafungia vioo hata siku moja,” alisema.

No comments