NISHA AWASHAURI WASANII KUEPUKA "FIGISUFIGISU" ILI KUPATA MAENDELEO

NYOTA wa filamu za vichekesho Salma Jabu "Nisha" amesema njia pekee inayoweza kuwafanya wasanii na watu wengine kupata mafanikio ni kuacha fitina na badala yake kuwa na wivu wa maendeleo.

“Jamani tusifanyie fitina wale ambao kila kukicha wanaaanda fitina za kiuwaharibia wenzao ninawashauri wawe na wivu wa maendeleo ili nao wafanikiwe,” alisema Nisha.

Alifafanua kuwa wivu wa maendeleo maana yake ni mtu kujifunza kwa mwingine aliyefanikiwa ili naye afikie hatua hiyo badala ya kufuata mbinu za kumharibia kama ilivyotokea kwake alivyopakaziwa kufanya biashara ya dawa za kulevya.


“Siuzi "unga" mimi ninafanya kazi za filamu na pia biashara mbalimbali halali lakini wasiotaka maendeleo yangu wanafanya kila mbinu kuniharibia ninawashauri wawe na wivu wa maendeleo.”

No comments