PAUL POGBA ATAMBA "WACHEZAJI WENZANGU MAN UNITED HUENDA WAMEROGWA"

KIUNGO wa Manchester United, Paul Pogba amewatambia wachezaji wenzake kuwa huenda wamefanyiwa vitendo vya imani za ushirikina na kujikuta wakitoka sare za mfurulizo nyumbani kwenye mchezo wa Ligi Kuu England.

Manchester hivi karibuni ikitoka sare dhidi Stoke City, Burnley, Arsenal na West Ham Ligi Kuu England na kufanya timu hiyo kusuasua.

Pogba alitoa pasi kwa Ibra wakati timu hiyo ilipofungana bao 1-1 na West Ham wikiend iliyopita.

Nyota huyo anaamini hivi karibuni nuksi hiyo ya sare inaweza kuondoka.

“Unajua tumeanza kuogopa kuwa huenda tumelogwa,” alisema Pogba.


“Kinachoogopesha ni kuwa timu tunazokutana nazo tunatawala mchezo na kujikuta tukitoka sare kama ilivyokuwa na Arsenal au West Ham.

No comments