PEP GUARDIOLA AWAFANYIA BARCELONA KITU MBAYA KAMA HAWAJUI VILE

MIAMBA wa soka nchini Uingereza timu ya Manchester City inayonolewa na kocha Pep Guardiola inahitaji kushinda mechi moja kufikia hatua ya mtoano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kupata ushindi wa kusisimua dhidi ya miamba Uhispania, Barcelona kwenye uwanja wake wa Etihad.

Guardiola ni kocha aliyeifanya Barcelona kuwa moja kati ya klabu bora kabisa barani Ulaya, kabla ya kuhamia Bayern Munich, laini usiku wa kuamkia jana ni kama alikuwa hawajui.

Mchezaji mwenye jina kubwa barani Ulaya kwa sasa, Lionel Messi wa Barcelona alifunga bao lake la 90 katika Ligi hiyo ya Mabingwa baada ya kupokea pasi kutoka kwa Neymar na kuwaweka mbele Barcelona muda wa mapumziko ulipokuwa unakaribia.

Lakini mambo yalibadilika upesi kabla ya kipyenga kupulizwa pale Sergi Roberto alipofanya kosa na Raheem Sterling akampa mpira Ilkay Gundogan ambaye alifunga kwa njia rahisi sana na kusawazisha.

City ambao walikuwa wanatafuta ushindi wao wa kwanza dhidi ya Barcelona katika mechi sita walizoanza kuthibitisha ubabe wao kuanzia wakati huo na free-kick ya Kevin De Bruyne ilimuumbua kipa Marc-Andreter Stegen dakika ya 51 na kuwa bao la pili.


Mpira wa Andre Gomes uligonga mwamba huku Barcelona wakisaka bao la kusawazisha lakini City walijihakikishia ushindi wa kusisimua dhidi ya klabu ya zamani ya meneja wao, Pep Guardiola, zikiwa zimesalia dakika 16 pale De Bruyne alipompa pasi Jesus Navas nae akatoa krosi iliyomfikia mshambuliaji Sergio Aguero aliyefunga.

No comments