PICHA 10: ISHA MASHAUZI, BI CHAU, KATARINA, ZIPOMPA KUKINUKISHA MWANZA LEO JIONI KATIKA "SAUTI YA MWANAMKE"


NYOTA wa taarab hapa nchini Isha Mashauzi leo atakuwa miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza kwenye tukio kubwa la kina mama lililopewa jina la “Sauti ya Mwanamke” litakalofanyika jijini Mwanza.

Sauti ya Mwanamke inafanyika katika hotel ya kisasa ya Gold Crest ikiwa imeandaliwa na Chocolate Princes Limited chini ya mwanadada Mboni Masimba.

Wasanii wengine watakaotumbuiza katika onyesho la Sauti ya Mwanamke ni Bi Chau, MC Zipompa, mchekeshaji Katarina na Zarry Edosha.

Shughuli hiyo itaanza saa itaanza saa 10 jioni hadi saa 5.30 usiku ambapo kiingilio ni shilingi 40,000 itakayokuwezesha pia kupata mlo wa jioni na zawadi kadha wa kadha.

Sauti ya Mwanamke pia itakuwa na mada mbali mbali kwaajili ya kuhimiza maendeleo ya kina mama katika nyanja mbali mbali za kiuchumi bila kusahau mambo ya ndoa na mahusiano.
 Shughuli Bi Chau akiwa Shekha ndani ya studio za Jembe FM Mwanza
 Bi Kutoka kushoto ni Zipompa, Katarina, Bi Fatma na Isha Mashauzi kwenye interview ya Jembe FM ya Mwanza
 Isha Mashauzi akijibu moja ya maswali
 Zipompa kwenye mahojiano na Jembe FM
 Mahojiano yakiendelea ndani ya Jembe FM
 Katarina na Isha Mashauzi 
 Mboni Masimba
Mwakilishi wa Precision Air ambayo inadhamini Sauti ya Mwanamke
Katarina na Zipompa

No comments