PICHA 10: MASHAUZI CLASSIC NA JAHAZI WALIVYOSHAMBULIA RUANGWA


ZIARA ya pamoja na bendi mbili bora za taarab hapa nchini, Jahazi Modern Taarab na Mashauzi Classic kusini mwa Tanzania, ilianza kwa kishindo katika mji wa Ruangwa Jumatano usiku.

Show hiyo ilipigwa katika ukumbi wa Yongolo ambapo Leyla Rashid na Isha Mashauzi walionyeshana kazi katika mpambano wao uliopewa jina la “Nani Zaidi”.

Pata picha 10 za onyesho hilo ambalo kwa namna nyingine lilithibitisha kuwa Jahazi bado iko imara kama chuma tofauti na ilivyokuwa ikitangazwa na baadhi ya watu kuwa bendi hiyo imekufa.
 Ma - Mc wa Jahazi na Mashauzi Prince Amigo (kushoto) na Hashim Said
 Isha Mashauzi akiimba mbele ya mashabiki wa Ruangwa
 Isha jukwaani
 Isha akitupa moja ya kete yake dhidi ya Leyla
 Jumanne Ulaya akikun'guta solo gitaa la Jahazi baada ya kurejea rasmi kundini
 Leyla Rashid akikamua moja ya nyimbo zake kali
 Leyla Rashid jukwaani
 Mishi Mohamed wa Jahazi akitesa jukwaani
 Asia Mzinga wa Mashauzi Classic akiimba "Ubaya Haulipizwi"
Leyla Rashid akiimba mbele ya mashabiki wake

No comments