PICHA 10: PRINCE AMIGO AFUNGUKA ILE MBAYA SHAM SHAM ZA PWANI ITV …atoa neno zito kuhusu Jahazi Modern Taarab


MWIMBAJI nyota wa Jahazi Modern Taarab Aboubary Soud “Prince Amigo” amefanya mahojiano ya aina yake na kipindi cha Sham Sham za Pwani cha ITV.

Mahojiano hayo ambayo yataruka Jumamosi hii saa 11 jioni na kurudiwa Jumatatu ijayo saa 5.30 usiku, yatatoa picha nzuri juu ya kinachoendelea ndani ya Jahazi Modern Taarab.

Amigo ambaye alikuwa akihojiwa na mtangazaji Hawa Hassan “Double H”, ameongoea mambo mazito na ya ndani kuhusu kundi hilo, ikiwa ni pamoja na kuweka wazi kuwa Jahazi bado iko hai.

Ili kujua kwa kina kile alichoongea Amigo, nini mipango ya Jahazi pamoja na kazi zijazo za kundi hilo, basi itupie macho Sham Sham za Pwani kupitia ITV Jumamosi jioni na Jumatatu usiku.
 Mahojiano ya Amigo na Sham Sham za Pwani ya ITV yakiendelea
 Wapiga picha wa Sham Sham za Pwani ya ITV wakiwa makini
 Amigo na Hawa Hassan
Amigo akisisitiza jambo
Amigo na Mtangazaji wa Sham Sham za Pwani ya ITV Hawa Hassan akimsikiliza Amigo kwa makini 
Kipindi kitaruka hewani Jumamosi saa 11 jioni na kurudiwa Jumatatu saa 5.30 usiku 
 Amigo akipangua maswali
 Amigo (kushoto) na Mtangazaji wa Sham Sham za Pwani ya ITV Hawa Hassan  
 Hawa Hassan (kulia) akifurahishwa na majibu ya Amigo
Hawa Hassan (kulia) akimtwanga swali Amigo


No comments