PICHA 10 ZA MASHAUZI CLASSIC WALIVYOSEPA NA KIJIJI KAOLE SNAKE PARK BAGAMOYO JUMAMOSI ILIYOPITA


MOJA ya show matata sana kutoka kwa Mashauzi Classic, chini yake Isha Mashauzi, ni ile iliyofanyika Jumamosi iliyopita mjini Bagamoyo kwenye ukumbi wa Kaole Snake Park.

Mashauzi likuwa kundi la kwanza kukata utepe wa burudani wa kiota hicho kipya cha maraha, likaangusha bonge la burudani lililoacha simulizi ya aina yake.

Ukumbi huo ulioko kilomita 5 kutoka Bagamoyo mjini, ukafurika vilivyo mashabiki waliozuuzika na waimbaji kama Abdulmalick Shaaban, Hashim Said, Zubeida Malick, Saida Mashauzi, Asia Mzinga na wengine kibao.

Kama ilivyo ada, nyota wa mchezo alikuwa Isha Mashauzi “Queen of the Best Melodies” ambaye aliiteka show kwa nyimbo zake kali zikiwemo “Viwavi Jeshi” na “Nimpe Nani”.

Pata picha 10 za wasanii wa Mashauzi wakiwa jukwaani kwenye ukumbi huo mkubwa kupindukia.
 Asia Mzinga jukwaani
Hashim Said akiimba "Bonge la Bwana"
Isha Mashauzi akishambulia na madansa wake
 Isha Mashauzi akiimba "Nimpe Nani" 
 Isha Mashauzi akisepa na kijiji
 Kali Kitimoto kwenye kinanda
 Mashabiki wakicheza kwa raha zao
  Mkude kwenye solo gitaa
 Rahma Aman mwimbaji chipukizi wa Mashauzi anayekuja juu kwa kasi
Saida Mashauzi akikupa kitu "Pendo la Ukakasi"

No comments