Habari

PICHA 18: ISHA MASHAUZI ALIVYONOGESHA TAMASHA LA SAUTI YA MWANAMKE MWANZA KWA KIINGILIO CHA SH. 40,000

on

JUMAPILI iliyopita Isha
Mashauzi aliwasha moto wa burudani jijini Mwanza katika tamasha la Sauti ya
Mwanamke lililofanyika katika hotel ya kisasa ya Gold Crest.
Tamasha hilo lililoandaliwa
na Chocolate Princes Limited ambalo lilikuwa maalum kwa kina mama tu, lilifana
sana licha ya kiingilio kikubwa cha shilingi 40,000.
Isha Mashauzi akiwa na bendi
yake ya Mashauzi Classic akapata fursa ya kutumbuiza nyimbo kadhaa zikiwemo
“Nimlaumu Nani”, “Nani Kama Mama” na “Nimpe Nani” na kufanya ukumbi ulipuke kwa
furaha.
Mbali na Isha Mashauzi,
kulikuwa pia na mada mbali mbali zilizotolewa ukumbini hapo huku mchekeshaji
Katarina akipata wasaa wa kuwavunja mbavu kina mama waliofurika Gold Crest
Hotel.
 Isha Mashauzi akiimba “Nani Kama Mama”
 Isha na wadau wengine wakisikiliza mada 
 Bi Chau akitoa mada ya ndoa
 Omar Seseme wa Super Kamanyola aliposhindwa kujiuzia na kukamata mpini wa solo wa Mashauzi Classic
 Mwanamke mashauzi bana asikwambie mtu!
 Isha Mashauzi jukwaani
Katarina akiwavunja mbavu kina mama
 Mama Ibra mmoja wa wanawake wajasiria mali aliyetoa mada nzito ya kibiashara
 Isha Mashauzi na wasanii wake jukwaani
 Mboni Masimba mwaandaaji wa Sauti ya Mwanamke akisema machache
 Hapa wadau wakicheza wimbo wa “Nimpe Nani”
 Isha Mashauzi akitupia masauti yake matamu
 Wadau wakilicheza goma la Mashauzi
 Mandhari ya ukumbi
 Sehemu nyingine inayooonyesha mandhari ya ukumbi
 Wadau wa Sauti ya Mwanamke wakifuatilia kwa makini kinachoendelea ukumbini
 Zipompa aliyekuwa MC wa Sauti ya Mwanamke akishuhudia mavituz ya Isha Mashauzi
 Waimbaji wa Mashauzi Classic Zubeida Malikc (kushoto) na Asia Mzinga wakifanya yao
Hii ni Gold Crest Hotel sehemu iliyofanyika “Sauti ya Mwanamke”

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *