PICHA 20: ISHA MASHAUZI NA LEYLA RASHID WALIVYOSEPA NA KIJIJI MTWARA


ILIKUWA ni hatari lakini salama! Mtwara ilipata habari yake kupitia mpambano wa Isha Mashauzi na Leyla Rashid Jumamosi usiku kwenye ukumbi wa Polisi Mess (Makonde Beach).

Wakali hao wawili wakiwa na bendi zao za Jahazi na Mashauzi Classic wakasababisha mbanano mkubwa ukumbini kwa namna mashabiki wa taarab walivyojitokeza kwa wingi.

Isha akakung’uta nyimbo tatu “Nani Kama Mama”, “Sura Surambi” na “Wiwavi Jeshi”  wakati Leyla aliibuka na “Kwahilo Hujanikomoa", “Nina Moyo sio Jiwe” na “Fanya Yako”.

Lakini ukiachia wawili hao, kulikuwa na mchuano pia kutoka kwa waimbaji wengine wa Jahazi kama Prince Amigo, Mwasiti Kitoronto, Fatma Kassim, Mishi Mohamed na Zubeida Mlamali dhidi ya waimbaji wa Mashauzi Hashim Said, Rahma Amani, Mariam Kasora, Aziza Binda na Asia Mzinga.

Kulikuwa pia na jambo moja la kuvutia sana kwa upande wa Jahazi kupitia mwimbaji wao mpya kabisa Hadija Mbegu ambaye aliukosha ukumbi mzima kupitia wimbo “Mtaniona Hivi hivi” au Maruperupe kama unavyofahamika na wengi.

Hadija aliukandamizia wimbo huo wa Fatma Mcharuko kwa usahihi wa asilimia 100 na kufanya ukumbi upagawe.

Zifutazo ni picha 20 za onyesho hilo la Isha na Leyla ndani ya Mtwara. Kesho utazipata za Lindi.
Asia Mzinga kutoka Mashauzi Classic
 Fatma Kassim wa Jahazi
 Hashim Said wa Mashauzi
 Ukumbi ukisalimu amri kwa Isha Mashauzi
 Isha Mashauzi jukwaani
 Isha Mashauzi akishambulia jukwaa
 Nyomi si la kitoto
 Kali Kitimoto mpiga kinanda wa Mashauzi
 Mwasiti Kitoronto wa Jahazi
 Leyla Rashid akifanya yake
 Leyla mbele ya nyomi la kufa mtu
 Leyla Rashid jukwaani
 Mariam mmoja wa waimbaji tishio sana kutoka Mashauzi
 Hadija Mbegu mwimbaji mpya kabisa wa Jahazi
 Isha akipozi na mashabiki wake wa Mtwara
 Mishi Mohamed wa Jahazi akiimba mbele ya umati wa mashabiki
Mishi akiendelea kutupia masauti matamu
 Emeraa Soloo (kushoto) akiwa na Prince Amigo wote kutoka Jahazi
Namba za hatari hizi ...Shaaban Kinanda (kushoto) na Mazoea ambao walifunika kabisa eneo la vinanda vya Jahazi


No comments