PICHA 23: MASHAUZI CLASSIC WALIVYOWASHA MOTO MORO, DODOMA, IGUNGA NA SINGIDA


Wikiendi iliyopita – Oktoba 28 hadi 31, kundi la Mashauzi Classic lilifanya kweli kwenye miji ya Morogoro, Dodoma, Igunga na Singida.

Kundi hilo linaloongozwa na Jike la Simba Isha Mashauzi “Queen of the Best Melodies”, lilipiga show ya kutakata katika ukumbi wa Kambarage ulioko Morogoro Ijumaa ya wiki iliyopita na kukonga nyoyo za mashabiki wengi, kabla ya kuelekea Dodoma siku iliyofuata na kuangusha burudani nzito katika ukumbi wa Perugina Club.

Baada ya onyesho lao ndani ya Dodoma, Mashauzi Classic wakapeleka uhondo mjini Igunga pale Sakao Modern Inn ambapo walisepa na kijiji kwa kuujaza vilivyo ukumbi huo.

Jumatatu ya Oktoba 31 (siku dume kiburudani), Mashauzi Classic wakajitosa katika ukumbi wa Scene Lodge Singida mjini na kufanya show iliyofana sana kiasi kwamba ilikuwa vigumu kuamini kuwa ilikuwa ni siku ya Jumatatu.


Pata picha kadhaa za Mashauzi Classic wakiwa jukwaani.
 Hashim Said ndani ya Morogoro
 Isha Mashauzi akisepa na kijiji ndani ya ukumbi wa Kambarage, Morogoro
 Isha akiendelea kukamua Morogoro
 Mariam anaendelea kuwa tishio ndani ya Mashauzi Classic
 Isha akiwanyoosha wakazi wa Moro
 Asia Mzinga akimpagawisha shabiki wa Igunga
  Asia Mzinga  akiimba "Ubaya Haulipizwi" ndani ya Igunga
 Nyomi linapokubali mbwembwe huwa hazikosekani ...Huyo ni Hashim Said pande za Igunga
 Isha Mashauzi mbele ya nyomi la Igunga
Isha akidhihirisha kuwa yeye ni Queen of the Best Melodies kwa wakazi wa Igunga
 Marim akikimbiza Igunga
 Isha akilamba nyekundu kwa mshabiki wa Igunga
 Igunga hiyo
 Uhondo wa Mashauzi unapokolea! huyu ni shabiki wa Igunga akionyesha ufundi wake
 Zubeida Malick jukwaani
 Asia Mzinga ndani ya Singida
 Isha katika muonekano mpya wa nywele mjini Singida
 Kali Kitimoto
 Singida hiyo
 Isha akifanya yake
 Rahma akikimbiza Singida
 Shabaan wa Kumwaga akilikamua bass gitaa
Zubeida Malick akifanya yake Singida ...si unaona buku tano tano zinachungulia pande flani

No comments