PICHA 6 ZA NAMNA ISHA MASHAUZI ALIVYOPOKELEWA MASASI …watu waziba njia ili asipite


ISHA MASHAUZI alipigwa na butwaa baada ya kupata mapokezi ya aina yake Masasi ambayo mwenyewe anadai yalimsisimua sana.

Baada ya wakazi wa Masasi kuona gari la Mashauzi Classic lililokuwa na chata za picha za Isha Mashauzi, walifanya kila juhudi kulisimamisha gari hilo ili wamsabahi Isha.

Mara gari liliposimama na Isha kuwasalimia kwa dirishani, wakazi hao wakataka ashuke na ili kutimiza adhma yao, mashabiki waliokuwa wakiendesha piki piki za kubebea mizigo (Toyo) wakazipanga piki piki hizo katika namna ya kuziba njia na kusema hawaziondoi hadi Isha ashuke.

Isha akashuka na kuwasabahi, ghafla watu wakazidi kuitana na kulijaza vilivyo eneo hilo lililokuwa jirani na kituo cha kikuu cha ma-bus ya mikoani.

Baada ya mashabiki hao wa Masasi kuridhika, waliruhusu msafara wa Isha uendelee.
 Mashabiki wa Masasi wakimtaka Isha ashuke ili wamsalimie
 Mara njia ikazibwa 
Hakuna kupita mpaka Isha ashuke kwenye gari
 Mashabiki wa Masasi wakizidi kusubiri Isha ashuke kwenye gari
Isha akashuka
Mashabiki wakafurahi mpaka basi

No comments