PROFESA JAY AZIDI KUMMEZEA MATE DIAMOND PLATNUMZ


MKONGWE wa muziki wa Kizazi Kipya, Profesa Jay ameendelea kupata somo kutoka kwa Diamond Platnumz, mara hii akisema kuwa anatamani ufanyaji kazi wa shujaa huyo wa taifa ambaye sasa ana ofisi yake maalum.

“Hivi sasa Diamond ana ofisi ambayo mtu akija anamkuta na sio baa kama sisi tulkivyokuwa tukifanya zamani. Sisi zamani ukimhitaji msanii kiofisi mnakutana baa mnasaini mkataba,” alisema Jay.

“Diamond ni msanii mkubwa na anaipeperusha bendera ya taifa kimataifa, ameamua kuwasaini wasanii wengine, yaani hataki kwenda peke yake, watu wanasema ukitaka kufanikiwa tembea peke yako ila ukitaka kufanikiwa zaidi ungana na wenzako wengi,” aliongeza.


Alisema kuwa kitendo cha Diamond kuwasaini wasanii Rich Mavoko, Raymond na Harmonize, kinampa changamoto kwavile ni watu anaorandana nao kwa aina ya muziki anaoufanya na pia ana nia ya dhati na muziki wa Tanzania kwa kuwasaidia vijana wenzake.

No comments