Q CHILLAH AMMIMINIA SIFA ALI KIBA... asema anastahili kuitwa "King Kiba"

MSANII mkongwe Q-Chillah amesema Ali Kiba anastahili kuitwa King Kiba na anaamini akikutana naye katika “Kolabo” watafanya kitu adimu ambacho kitawashtua mashabiki kwa madai kwamba wawili hao ni wakali wa sauti.

Alisema yeye na Kiba ni wakali kwenye muziki wa Kizazi Kipya ndiyo maana ana uhakika wakikutana wanaweza kutoa wimbo mkali na kuwashangaza mashabiki.

“Ali Kiba anastahili kuitwa King Kiba kwa sababu anafanya vizuri na pia mimi napenda ngoma zake ila kuna utofauti kati yangu na yeye ila kutokana kwenye kolabo  ni lazima tufanye wimbo wa tofauti sana kwa kuwa sisi wote ni wakali wa sauti,” alisema.


Alisema kuwa tangu aanze muziki hajawahi kumpigia msanii yoyote hapa nchini akiomba kufanya kolabo lakini yeye anakuwa akipokea simu nyingi kutoka kwa wasanii mbalimbali wakimuomba kumshirikisha katika nyimbo zao.

No comments