RAYVANNY AFUNGUKA NA KUSEMA ALIDHARAULIKA SANA KABLA YA KUFANIKIWA

MSANII anayekuja juu kwa kasi kwenye muziki wa Kizazi Kipya, Rayvanny amesema kuwa amewahi kukutana na changamoto nyingi zikiwemo za watu kumdharau wakimuona kama “mla unga”.

Alisema kuwa dharau hizo hazimkatisha tamaa na asa ameanza kuona mafanikio ya kipaji chake kupitia muziki na ana uhakika waliomdharau wakati huo watakuwa wameanza kumheshimu.

“Huwa sina muda wa kupoteza katika muziki ndio maana sikukata tamaa nilipokuwa nikidharauliwa kwamba nafanya kazi ambayo haiwezi kunifikisha kokote, lakini sasa nimeanza kuonja matunda ya uvumilivu wangu,” alisema.


Rayvanny anayetamba na nyimbo mbalimbali zikiwemo za “Kwetu” na “Natafuta Kiki”, alisema aliwahi kutoa wimbo uitwao “Mwenyewe” lakini kwa bahati mbaya haukufanya vizuri lakini hakukata tamaa licha ya kusemwa kuwa hana lolote zaidi ya kula unga.

No comments