REAL MADRID "PUNGUFU" KUGALAGAZANA NA WARSAW BAADAE LEO

REAL Madrid haijawahi kufungwa na timu kutoka Poland katika mechi saba za michuano ya UEFA, wanakutana leo kucheza dhidi ya Legia Warsaw watakaokuwa nyumbani mjini Warsaw kwenye uwanja wa Jeshi la Poland.

Kutokana na hilo, kocha Zinedine Zidane amewaacha benchi nyota wake James Rodrguez na Marcelo.

Rodriguez ameachwa pamoja na kwamnba amekuwa akicheza mechi nyingi za Ligi ya Mabingwa.

Marcelo pia ameachwa kwenye safari hiyo na kutokuwepo kwa mabeki majeruhi Pepe na Sergio Ramos kumelazimu majukumu yao kuzibwa na Nacho na Raphael Varane.

Legia Warsaw ni moja kati ya timu tatu kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa ambazo zimepoteza mechi zote tatu za mwanzo hatua ya makundi. Vibonde wengine ni Club Brugge na Dinamo Zagreb.

Real Madrid inakutana na wapinzani wao hao ambao katika mchezo wa kwanza waliwanyuka mabao 6-0 mjini Madrid.
Lakinbi pia vibonde hao waliogelea na kipigo cha mabao 5-1 kutoka Dortmund.

Hivyo mechi ya leo ambayo Real Madrid wamepangua kikosi huenda wasiwe na kazi nzito kupata ushindi kutokana na rekodi mbovu ya vipigo kwa timu hiyo ya Poland.

Baada ya Los Branca kwenda sare mara nne katika mashindano yote, wamerudi na kasi nzuri wakishinda mechi tano na kukusanya mabao 24.


Miamba hiyo ya Hispoania kwa sasa wako nafasi ya pili kundi F wakiwa sawa kwa pointi na Borussia Dortmund.

No comments